Ujenzi wa majumba ya kisasa na yenye muonekano wa kipekee unafanyika kila siku, na biashara imetajwa kuwa sababu kubwa zaidi kwenye kuleta ushindani. Leo January 11, 2016 CCN imezitaja nyumba 12 zilizoweka rekodi ya kuwa na gharama kubwa zaidi duniani mwaka 2016.
Mjengo huu una vyumba vya kulala 32, swimming pool iliyojengwa kama ziwa lenye maji mengi, sehemu ya kukinga Wine, pamoja na bustani za kila aina, jumba hili liliwahi kutajwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu UNESCO kama bustani bora ya dunia
2. 301 N Carolwood Drive, California – MAREKANI (Zaidi ya Tsh. Bilioni 222).
Mjengo mwingine nii huu kutoka California, uko kwenye eneo la ukubwa wa futi za mraba 30,000 huko Los Angeles, uliuzwa kwa bilionea Tom Gores mwezi October 2016. Una vyumba 10 vya kulala, bafu 20, uwanja wa Basketball, gereji 10 na hapo ulikuwa umepungzwa kwa dola milioni 50 kutoka bei ya mwanzo.
3. The Playboy Mansion, California – MAREKANI (Zaidi ya Tsh. Bilioni 222).
Wakati watu wakishangaa bei iliyotangazwa juu ya kuuzwa nyumba hii ambayo ilikuwa zaidi ya dola za Marekani Milioni 200m, alijitokeza bilionea Daren Metropoulos na kuinunua kwa dola milioni 100 mwezi August 2016. Ndani yake kuna ukumbi wa kisasa wa Cinema, nyumba ya pembeni kwaajili ya wageni, Zoo yenye leseni kwaajili kuhifadhi wanyama pori.
4. Crespi Hicks Estate, Texas – MAREKANI (Zaidi ya Tsh. Bilioni 222).
Likiwa limepambwa na sakafu ya Mable kwenye njia zake, hili lilikuwa jumba lililouzwa bei kubwa zaidi kwenye mji wa California, Marekani. Jengo hili liko kwenye eneo la ukubwa wa futi za mraba 28,000 huko Dallas na lilinunuliwa na muanzilishi wa kampuni ya Beal Bank, Andrew Beal mwezi January 2016.
Pamoja na muonekano wa ukubwa huo lina vyumba 7 tu vya kulala. Pia inatenganisha nyumba ya wageni na wenyeji.
5. The Penthouse, 432 Park Avenue, New York – MAREKANI (Zaidi ya Tsh. Bilioni 194).
Hii ni nyumba ya ndani (Apartment) iliyoweka rekodi ya mauzo makubwa jijini New York Marekani mwaka 2016. Ikiwa ndani ya eneo la ukubwa wa futi 8,255 za mraba ndani ya jengo refu zaidi la makazi ya watu jijini humo, Michoro ya ramani zake imebuniwa na mtaalamu wa majengo Rafael Viñoly, ilinunuliwa na bilionea kutoka Saudi Arabia, Fawaz Al Hokair mwezi September 2016.
Picha nyingine za majumba yaliyotajwa kuwa na bei zaidi duniani mwaka 2016.
Source: CNN
VIDEO: Ilikupita hii ya nyumba mpya aliyoinunua Diamond Platnumz South Africa? Bonyeza play hapa chini kutazama.