Baada ya kuwepo taarifa za njaa na ukame uliosababishwa na ukosefu wa mvua kwenye maeneo mengi nchini, leo January 16, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amelazimika kutoa ufafanuzi kuhusu hali ya chakula nchini huku akisisitiza kuwa Tanzania ina chakula cha kutosha na haina shida ya njaa.
Waziri Tizeba amesema kuwa watu wanaoeneza taarifa za kuwepo kwa njaa Tanzania wana lengo la kuingiza mahindi yao yasiyo na ubora ili wafanye biashara, jambo ambalo serikali imelikataa.
Akizungumzia uhalisia wa hali, amesema kilichotokea ni kupanda kwa bei ya mahindi, hali iliyosababishwa na uamuzi wa serikali kuuza nafaka hiyo katika mataifa jirani yaliyokuwa na uhitaji mkubwa, ingawa kiwango kilichouzwa kilikuwa ni sehemu ya mahindi ya ziada.
“Mwaka jana gunia la mahindi kwa bei ya wastani wa kitaifa ilikuwa 65,000 lakini sasa ni 85,000 na wala haijafikia mara mbili mara tatu kama inavyosemwa ingawa kuna maeneo kama rorya imefikia hadi 150,000 kutokana na wao kutegemea misimu miwili wakajikuta wanatumia akiba yao lakini hali ya hewa ikawa tofauti kwahiyo kuna wafanyabishara wakaamua kutumia hiyo fursa kupandisha bei zaidi”
“Mavuno ya nafaka yalikuwa tani milioni 16 wakati mahitaji yakiwa tani milioni 13 kwahiyo ziada ilikuwa tani milioni 3, kwahiyo katika hiyo ziada milioni 1.5 ikasafirishwa nje, wenzetu walikuwa wananunua kwa gharama yoyote kwa kuwa walikuwa na shida, hiyo ndiyo maana bei ya nafaka imepanda sana hasa mahindi, kwa sasa bei imefika hadi mia 8 mia 9 na wauzaji ni walewale, kwahiyo hawezi kuuza ndani kwa bei ya chini lakini kupanda huko kulitarajiwa” – Waziri Charles Tizeba
Kuhusu ukame, amesema ni kweli kuna hali ya upungufu wa mvua, na hiyo inafahamika maana ilishatabiriwa na kuwataka wananchi watunze akiba yao ya chakula na wasidanganyike kukiuza, kwa sababu hali ya hewa haitakuwa nzuri katika baadhi ya maeneo.
Amewasihi wananchi waache tamaduni ya kung’ang’ania chakula cha aina moja na kuwataka kutumia vyakula vingine kama mahindi yamepanda bei.. “Nafaka siyo mahindi tu, tunao mchele na mpunga wa kutosha, na viazi vipo kutoka Tunduma, watumie hivyo”
Waziri Tizeba huyo amepiga marufuku mtu yoyote kutoa taarifa za njaa kwa kuwa serikali ndiyo inayojua hali ya chakula kupitia vyanzo vyake.
Kufahamu kila kitu alichozungumza Waziri Tizeba, bonyeza play hapa chini kutazama.
VIDEO: Yapo hapa Magazeti yote ya leo, na David King ameyachambua yote. Unaweza kutazama hapa chini.