Nafahamu wapo wale ambao kutunza kumbukumbu ya vitu vya zamani ni kazi ngumu sana, lakini nimeona mara nyingi ikitokea kwa watu maarufu wanapofariki basi vile vitu vya kipekee ambayo walivitunza kama kumbukumbu kwenye maisha yao vinapouzwa kwenye minada huwa na gharama kubwa sana.
Kutoka Afrika Kusini nimeipata hii kuhusu barau ambayo iliwahi kuandikwa na bondia maarufu duniani hayati Muhammad Ali kwenda kwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela akitoa salamu za pole ya msiba wa wa mmoja wa viongozi muhimu wa chama cha A.N.C, Chris Hani, Barua hiyo imepigwa mnada na kuuza kwa paundi 7,200 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 19.5.
Barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na bondia “Muhammad Ali alipotembelea nchini Afrika Kusini mwaka 1993, Barua hiyo ilichpwa na mchapaji maarufu kutoka hotel ya Elangeni iliyopo jijini Durban, ambako bondia huyo alikuwa akikaa kwa wakati huo.
VIDEO: Alice Tupa amekuchambulia Magazeti yote ya leo December 18, 2016. Nimeshayaweka hapa bonyeza play kutazama