Kutoka Kenya leo January 11, 2017 nimekukusanyia hizi picha 10 zikionesha muonekano wa nje wa iliyokuwa ngome ya utawala wa Ureno wakati wa ukoloni. Ngome hii inapatikana kwenye visiwa vya Mombasa nchini Kenya, iko umbali wa kilomita 490 kutokea jiji la Nairobi.
Fort Jesus (Ngome ya Yesu), ilijengwa na wakoloni wa Kireno kuanzia mwaka 1593 hadi 1596 ikiwa na ramani iliyochorwa na mbunifu wa majengo “Giovanni Battista Cairati” kwa lengo la kulinda bandari ya Mombasa, ngome hii inafananishwa na ngome za taifa la Ureno zilizokuwepo karne ya 16 zikitumiwa na jeshi la nchi hiyo.
Ukubwa wa eneo ilipojengwa ngome hiyo unatajwa kufikai hekta 2.36 zikijumisha eneo la majengo na mazingira yake.
Nimekuwekea hapa picha 10 za jengo hilo kutoka Kenya.
VIDEO: MAGAZETI: IMF yaeleza hali ya uchumi waTZ, Manusura wasimulia ajali ya Jahazi Tanga. Bonyeza play kutazama.