Habari za Mastaa

Utapenda alichokiandika Ne-Yo kuhusu collabo yake na Diamond Platnumz

on

Inaweza kuwa ngeni kidogo kwenye masikio yako lakini tambua kwamba hii ni kati ya single kubwa sana duniani, Star mwimbaji wa kimataifa Ne-Yo kutoka Marekani ameendelea kuonesha jinsi anavyomkubali star wa BongoFlava Diamond Platnumz baada ya kupost cover ya wimbo aliopiga naye collabo “Marry You”.

“Upendo wa kutosha kwa mshikaji wangu @diamondplatnumz msanii mkali na rafiki yangu kutoka Africa! Itafute single aliyoifanya na mimi #MARRYYOU inapatikana sasa kwenye iTunes. #NEWMUSIC ?????????,” – Ne-Yo.

Kupitia Instagram, Ne-Yo ameandika maneno ya kuifanyia promotion collabo hiyo huku akimtaja Diamond “Simba” kama msanii mkali na rafiki yake mkubwa kutokea barani Afrika, single hiyo unaiweza kuipata kwa kudownload kupitia >>> itunes

neyo

VIDEO: Mastaa wengine ambao Diamond Platnumz amezungumza kufanya nao kazi ni hawa, Bonyeza play hapa chini kutazama.

Soma na hizi

Tupia Comments