Leo January 19, 2017 kutoka IKULU Dar es salaam, Tanzania Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Martin Bille Herman.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Denmark hapa nchini Einar Hebogard, Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.
Martin Bille Herman amesema katika mazungumzo hayo wamejadili kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Denmark na pia wamekubaliana kuuimarisha zaidi hususani katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Mkapa amesema lengo la kukutana na Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kumpa taarifa juu ya kazi anayoendelea kuifanya ya kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.
Nimekuwekea hapa picha zote kutoka IKULU.
VIDEO: Ulipitwa na hii ya Waziri Mkuu alivyomaliza mgogoro ulioanza kusuluhishwa tangu 1997, Nimekuwekea hapa.