Wakati mwaka 2016 ulipokaribia mwishoni kulitokea vurugu kati ya wakulima na wafugaji huko wiliyani Kilosa mkoani Morogoro, sababu ikatajwa kuwa wafugaji wanaoingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima kitu kilichosababisha wengi wao kukatwa mapanga na kuchomwa mikuki.
Leo January 3, 2017 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amefika katika kijiji cha Tindiga kilichopo wilaya ya Mikumi zilipotokea vurugu zilizopelekea mkulima mmoja kuchomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni na kusikiliza kero zinazowasumbua wananchi wa Kilosa kabla ya kutoa maamuzi.
Waziri Mwigulu amesema kuanzia sasa likitokea tukio lolote la watu kuuana kwa mapanga, mikuki, sime na silaha zozote za jadi zinazotumiwa hasa na wakulima na wafugaji, serikali itafuta utaratibu wa kubeba silaha hizo na atakayebeba atakamatwa na kuchukuliwa hatua kama watuhumiwa wengine.
Kinginie alichoagiza Waziri Mwigulu ni wakuliam na wafugaji kwa pamoja kuwakamata watu wote watakaohusika na kuanzisha vurugu na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola kabla jeshi la polisi halijafanya maamuzi yake.
Waziri Mwigulu amesema likitokea tukio la wakulima na wafugaji kuuana kwa silaha za jadi, serikali itafuta utaratibu wa kubeba silaha hizo pic.twitter.com/fmXFkgS9RR
— millardayo (@millardayo) January 3, 2017
MOROGORO: Waziri Mwigulu amewaagiza wakulima na wafugaji kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola watu watakaohusika na mashambulio pic.twitter.com/fHrQ2pcJHa
— millardayo (@millardayo) January 3, 2017
VIDEO: Ulipitwa na alichokisema mkulima aliyechomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni baada ya kuanza kufanyiwa upasuaji? Tazama video hii.