Michezo

Kinda wa Ghana mwenye ndoto ya kuichezea Korea Kusini

on

Mwanasoka chipukizi wa Ghana Dennis Osei ,17, ametangaza kuwa na ndoto ya kuichezea timu ya taifa ya Korea Kusini kwa miaka ya baadae.

Osei kwa sasa ni sehemu ya timu ya Kyemyung High Soccer School , alienda Korea akiwa na umri wa miaka 7 na maisha yake yote amekuwa akiishi Korea na ataruhusiwa kuwa na Passport ya Kikorea akifikisha umri wa miaka 19.

Dennis Osei anayetajwa kama ndio mchezaji soka kutoka Soccer School nchini Korea kuwa na kasi sana uwanjani, ameibuka mfungaji bora wa jimbo la Gyeongsang.

“Nataka kuwa mchezaji mkubwa na kushinda Ballon d’Or siku moja watu wanasema mimi tayari kama Mkorea tu na nakubaliana na hilo sababu nimeishi hapa kwa muda mrefu na nimejifunza kila kitu kuhusu Korea, ningependa kuichezea Korea na kuichezea Ghana”>>> Osei VIA Arirang TV

Soma na hizi

Tupia Comments