Habari za Mastaa

VIDEO: Kama ulitumiwa taarifa za kifo cha Mr. Nice, hii ukifikie kutoka kwa mama yake

on

Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba msanii wa siku nyingi wa bongofleva Mr. Nice amefariki na mwili wake upo Hospitali ya Taifa Muhimbili. AyoTV imempata Mama Mzazi wa Mr. Nice nyumbani kwa msanii huyo Kibamba Dar es salaam.

“Kusema ukweli hayo mambo yalisemwa lakini mimi nilizungumza na mwanangu live akasema yeye ni mzima wa afya mimi sikusikia kwenye vyombo vya habari nilisikia watu wakisema ndio nikataka anipigie simu ili niweze kujua hali yake ikoje. Alinipigia tukazungumza” – Mama Mr. Nice

Kujua kila kitu alichokisema mama wa Mr. Nice kuhusu taarifa hizo, nimekuwekea video hapa chini.

VIDEO: Ilikupita hii ya BIRTHDAY ya muigizaji Irene Uwoya kulivyohappen, mastaa waliofika je? Tazama video hapa chini.

Soma na hizi

Tupia Comments