Habari za Mastaa

Maneno 104 ya Profesa Jay aliyomwandikia rapa Darassa.

on

Kitu pekee ambacho kilibakia kukipata kwenye muziki wake ni kukubalika na kuheshimika, Rapa Darassa mkali wa hit single za Too Much na Muziki bila shaka sasa anakipata kitu hicho kutoka kwa mashabiki wake na mastaa wakongwe kwenye game ya BongoFlava na Hip Hop Tanzania.

Pamoja na kuwepo kwenye game kwa muda mrefu kidogo, ni ndani ya mwaka 2016 kila kitu kinaanza kubadilika kutoka kwa rapa huyu. Darassa amezishika headlines za kila sehemu kuanzia kwenye social media, radio na tv karibia zote Afrika Mashariki kwasasa stori kubwa ni Darassa kuwa “Too Much” na “Muziki” wake.

Tayari wakongwe wengi wameshawasha taa za kijani kuonesha kukubali alichokifanya rapa huyu wapo pia Afande Sele, Mwana FA na wengine wengi, lakini leo nimeipata hii pia ya Hip Hop legend Profesa Jay ambaye kwasasa ni Mbunge wa Mikumi, amepost maneno yake kuhusu juhudi na mafanikio aliyoyapata Darassa.

“Mdogo wangu @darassacmg Imani yako, Kutokukata tamaa na Struggle yako ya Usiku na Mchana ndio imekufanya ufikie hapo ulipofikia, Nakumbuka wakati unashoot Wimbo wako wa USIKATE TAMAA uliniambia unatamani ufikie level za juu kama zetu, Nami nilikwambia hakuna kinachoshindikana chini ya JUA Ukiset GOALS, kufanya kazi kwa bidii na SALA yote Yanawezekana.”

“Naamini kwa style hii ya JIWE juu Ya JIWE, NDOTO yako inakwenda kuwa kweli, Cha MSINGI usiridhike na mafanikio haya..HUU ni mwanzo tuu na mafanikio makubwa zaidi yako at your DOOR, Keep your eyes open and Keep ya HEAD UP, SKY IS THE LIMIT, GO GET DEM… BLESS #ACHA MANENO WEKA MUZIKI @darassacmg @darassacmg” – Profesa Jay

jay

VIDEO: LIVE kwenye jukwaa la After School Bash huyu hapa ni Darassa akiperform hit single “Too Much na Muziki”. Tazama hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments