Siku 18 zikisalia kuelekea kuumaliza mwaka 2016, bado kunaendelea kuwepo matukio yenye utata likiwepo hili kutoka Heka Heka ya Leo Tena ndani ya Clouds FM ambayo iko na stori kuhusu dereva bajaji aitwaye Michael kutoka ndani ya jiji la Dar es salaam ambaye ametoweka bila kuwepo taarifa yoyote.
Kwa mujibu wa dereva bajaji maarufu kwa jina la Kiranga ambaye walikuwa wanafanya kazi naye kwenye kituo kimoja ameeleza kilichotokea.
“Yaani hapa jinsi ilivyokuwa mimi nilitumiwa meseji kwamba Michael hayupo tokea jana aliaga anaenda kwake lakini hajafika basi mimi nakafika asubuhi pale lakini hatukufatilia siku ile tuliamua kusubiri kuona kama atarudi lakini hakurudi, lakini zilivopita siku 3 ikabidi niende kuripoti polisi Oyesterbay”
“Polisi walitwambia tuendelee kumtafuta kwenye vituo vya vyote vya polisi, hospitali na mochwari ili kujihakikishia kama tutampata, tumeenda kwote huko lakini tumemkosa. Sisi tunahofu kubwa kwasababu hatujui amepatwa na nini mpaka sasa” – Kiranga
Wakati huo huo mke wa dereva bajaji huyo naye ameelezea mazingira ya siku ambayo mume wake alitoweka nyumbani kwa mujibu wa taarifa ya majirani, yeye pia alikuwa msibani hivyo hakurudi nyumbani.
“Majirani wanasema kwamba siku ambayo mimi sikuwepo alirudi usiku akalala na alishinda nyumbani mpaka jioni, baada ya siku mbili mimi nikarudi nikamuulizia wakanambia baba Fredy hayupo ila alishinda pale akifua nguo zake hiyo ilikuwa Jumapili nikaamua kumpigia simu kumwambia mimi narudi akaniuliza kama aje kunichukua nikasema narudi Jumanne, imefika hiyo siku nampigia tena hapatikani” – Mke wa Dereva Bajaji
Kuipata Full Stori bonyeza play hapa chini.
VIDEO: Ilikupita hii ya Said aliyetobolewa macho na Scorpion siku alipokutana na Diamond Platnumz? Itazame hapa chini.