Habari za Mastaa

Rekodi nyingine Drake na Wizkid wameivunja kwenye mtandao wa Spotify

on

Baada ya mastaa Drake na Wizkid kukutana kwa mara ya pili kwenye collabo ya “One Dance” single hii imeendelea kufanya maajabu kwenye charts kubwa za muziki duniani. Mzigo ukiwa unapatikana kwenye albam ya Darke Views” umekuwa wimbo wa kwanza kwenye mtandao wa kuuza nyimbo wa Spotify kusikilizwa zaidi ya mara billioni moja kwa mujibu wa Billboard.

Hiki ni kitu kingine kikubwa kwa rapa huyu anachojivunia kumaliza nacho mwaka 2016. Mwezi September mwaka huu, albam ya Views ilikuwa albam ya kwanza kufikisha wasikilizaji billioni moja kupitia Apple Music. Views pia iliingia kwenye top slot ya mtandao wa Apple na kuongoza idadi ya albam 25 zilizofanya vizuri mwaka 2016, wakati single ya “One Dance” ikiongoza chart ya nyimbo bora 25.

Kwa sasa albam ya Views imepewa tuzo ya kufikiza mauzo makubwa zaidi ya mara nne na taaisi ya RIAA na kumsaidia Drake kuwania tuzo nane Grammy. Na hiyo haijamfanya jamaa arelax, tayari Drake ametanagza ujio wa albam yake mpya “More Life”, inayotarajiwa kutoka mapema mwaka 2017.

VIDEO: Niliipata hii Full Video ya Wizkid alipokuja Tanzania na kupanda kwenye Steji ya FIESTA2016 CCM Kirumba, Mwanza. Itazame hapa

Soma na hizi

Tupia Comments