Leo January 17, 2017 imetoka ripoti ya makusanyo ya kodi katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa Fedha 2016/17 kuanzia Julai hadi Disemba 2016, ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kodi jumla ya shilingi trilioni 7.27 ikilinganishwa na shilingi trilioni 6.44 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2015/16.
Taarifa hiyo inaonesha ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia 12.74.
Mlinganisho wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 ni kama ifuatavyo:
MWEZI | MWAKA 2015/16 | MWAKA 2016/17 | Ongezeko |
JULAI | 925,384.7 | 1,069,458.5 | 15.57 |
AGOSTI | 923,316.9 | 1,154.222.5 | 25.01 |
SEPTEMBA | 1,132,310.3 | 1,378,048.9 | 21.70 |
OKTOBA | 1,037,179.8 | 1,131,094.9 | 9.05 |
NOVEMBA | 1,027, 939.6 | 1,123,509.7 | 9.30 |
DISEMBA | 1,403, 189.8 | 1,414,921.8 | 0.84 |
JUMLA | 6,449,321.1 | 7,271,256.26 | 12.74 |
Jitihada mbalimbali zinafanywa ili kuhakikisha TRA inaongeza makusanyo kwa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kufuatili, kuhimiza matumizi ya mashine za kielektronik na kuhimiza ulipaji wa kodi ya majengo.
TRA inaendelea kuhimiza wafanyabiashara wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuwasilisha ritani za VAT kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi kama ilivyobadilishwa katika Sheria ya Fedha ya 2016.
Pamoja na hayo tunawakumbusha na kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam ambao hawajafanya uhakiki wa taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 31 Januari 2017 ili zoezi hilo liweze kuanzishwa katika mikoa mingine.
TRA inatoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati ili serikali ipate mapato yake ambayo yataiwezesha kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.
Kwa wafanyabiashara wenye madeni ya nyuma wanashauriwa kujitokeza kuonana na Mameneja wa Mikoa na Wilaya kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni yao bila kuathiri biashara zao.
Wamiliki wa majengo wanaaswa kutoa ushirikiano kwa kulipia ankara zao za kodi ya majengo kwa hiari .
VIDEO: Ilikupita hii ya sababu za Rais Magufuli kuivunja Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA? Niko nayo hapa chini.