Habari za Mastaa

MTV BASE wamesema hii ndio list ya nyimbo 20 kali za Nigeria 2016 (+Full List)

By

on

Kama ilivyo kawaida mwaka 2016 unaenda mwishoni, tayari media zinaanza kutoa tathmini yake kwenye masuala mbalimbali ikiwemo hii ya kituo cha Televisheni cha MTV Base kuitaja list ya ngoma 20 walizodai ndio zimefanya vizuri zaidi nchini Nigeria kwa mwaka 2016.

MTV BASE wameanzisha HashTag ya #BaseHottestNaijaTracks2016 kwenye mtandao wa twitter na kuzitaja nyimbo za wasanii kutoka Nigeria zilizotengeneza chart za radio na tv nchini humo na kuitambulisha rasmi listi hiyo ya “Best Nigerian Songs of 2016”.

List hiyo imepangwa na panel ya majaji wanaotajwa kuujua muziki na ni wadau wakubwa kwenye music industry ambao wamechaguliwa kutoka kwenye vituo vya radio vyenye nguvu zaidi Nigeria, watangazaji wa TV na Radio, waandishi wa habari,, bloggers pamoja na watu wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mwaka 2016 majaji wa MTV BASE walikuwa ni: Senior Associate, Pulse NG, Ayomide Tayo; Publisher, Mystreetz Magazine, Sesan Adeniji; OAP 97.3 Classic FM, Buki Sawyerr Izeogu; OAP Beat 99.9 FM, Douglas Jekan; A&R Entertainment Consultant, Bizzle Osikoya; Meneja wa wasanii na CEO Stargaze Management Company, Asa Asika pamoja na mtangazaji wa zamani wa MTV Base na kituo cha radio cha City FM, Cynthia “Cvon” Okpala.

Kitu kilichoshtua watu ni kutokuwepo kwa majina wasanii wakubwa naliohit sana mwaka huu kama vile Wizkid, Davido, Tiwa Savage, Lil Kesh na Yemi Alade.!!!

Ni hii ndio list ya wasanii na nyimbo zao zilizotajwa kuwa kali zaidi kwa mwaka 2016.

image

Nimekuwekea hapa FULL LIST ya ngoma zote 20 zilizotajwa na MTV Base kama #BaseHottestNaijaTracks2016

 1. Phyno ft. Olamide – Fada Fada
  2. Tekno – Pana
  3. Olamide – Who You Epp
  4. Kiss Daniel – Mama
  5. Reekado Banks – Oluwa Ni
  6. Adekunle Gold – Pick Up
  7. Ycee – Omo Alhaji
  8. Sugarboy – Holla Holla
  9. Patoranking ft. Sarkodie – No Kissing
  10. Mr Eazi ft. Efya – Skin Tight
  11. D’banj – Emergency
  12. Koker – Kolewerk Remix
  13. Humblesmith – Osinachi Remix
  14. Mayorkun – Eleko
  15. Timaya ft. Flavour – Money
  16. Tekno -Where
  17. Falz ft. Davido x Olamide – Bahd Baddo Baddest
  18. Zoro ft. Flavour – Ogene
  19. Niniola – Shabba
  20. Ajebutter ft. Falz – Bad Gang

Baada ya kumaliza kuisoma hii list bila shaka unayo comment yako tafadhali usiache kuniandikia hasa kwa kuona mastaa kama Wizkid, Davido, Tiwa Savage, Lil Kesh, Yemi Alade hawapo kwenye list hii.

VIDEO: AYO TV imempata Christian Bella na amekanusha kabisa kwamba kuna kazi yoyote ameifanya na Davido. Tazama hapa chini

VIDEO:

Soma na hizi

Tupia Comments