Huko Kilimanjaro wilaya ya Moshi kuna moja kati ya matukio ya nadra kukutokea katika familia, baba mzazi wa mmoja wa maharusi mwishoni mwa wiki iliyopita aliibuka kanisani saa chache kabla ya muda uliopangwa kufunga harusi, na kuweka pingamizi la ndoa, Maharusi waliopatwa na mkasa huo ni Yohana Mohammed na Rose Sembeye.
Kitendo cha mzazi wa Yohana kuweka pingamizi kilisababisha maharusi wote wawili kupoteza fahamu, na licha ya harusi kutofungwa, wawili hao waliamua kwenda ukumbini kuungana na waalikwa saa 11:00 jioni wakitokea hospitalini ambako walikuwa wamepumzishwa.
Ayo TV imemtafuta Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Joseph Posta, Dar es salaam Dk. Joseph Matumaini kutueleza taratibu zikoje katika mapingamizi kabla ya ndoa kufungwa.
“Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inataka watu ambao wanataka kufunga ndoa waiandikishe kwanza na itangazwe kwa siku 21 ili umma utambue kwamba na ndoa inakuja endapo kuna sababu maalumu zinazowahusu basi RITA watatoa taarifa ya siku 7 kwa kanisa ambalo lina wasimamizi wake ambao ni mapadri.” – Paroko Dr. Joseph Matumaini
VIDEO: Mwanamke aliyeingia kanisani na kupinga kufungwa kwa ndoa akidai bwana harusi ni mume wake. Tazama hapa chini