Mix

Picha 9: Rais Magufuli alivyowaapisha watumishi wengine wa Serikali Ikulu DSM

on

Leo December 23, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewaapisha viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Majaji wa Mahakama ya Rufani.

Walioapishwa ni Jaji Semistocles Simon Kaijage anayekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid anayekuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Jaji Harold Reginald Nsekela aliyeapishwa kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Viongozi hawa watashika nyadhifa hizo kwa kipindi cha miaka mitano.

Kwa upande wa Majaji walioapishwa ni Jaji Rehema Kiwanga Mkuye, Mhe. Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi, Jaji Dkt. Gerald Alex Mbonimpa Ndika, na Jaji Jackobs Casthom Mwatebela Mwambegele.

10hgsgsgsgsnec

unnamed1 unnamed-1 unnamed-6 unnamed-9 unnamed-22 unnamed-31 unnamed-42

VIDEO: Ulipitwa na majibu ya Rais Magufuli kwa wanaosema yeye ni Dikteta? Tazama video hapa chini.

Soma na hizi

Tupia Comments