Mtuhumiwa Elisha Mkoko mwenye umri wa miaka 20 alikuwa akijishughulisha na kazi ya Kinyozi na alikuwa akifanyia vitendo hivyo hapohapo kazini kwake eneo la Mtwivila.
Kesi hiyo ilikuwa na Mashahidi 7 akiwemo Mwalimu wake aliyegundua kuwa Mtoto huyo anatoa harufu ndipo akatoa taarifa kwa uongozi wa Shule na baadaye uongozi wa Mtaa na alipopelekea Hospitali vipimo vya Daktari vilionesha Mtoto huyo ana michubuko iliyoonesha kuwa Mtoto huyo alikuwa ameingiliwa kinyume na maumbile.
Mtoto huyo alikuwa akiishi na Bibi yake kwasababu Baba yake ni Mtu wa kusafiri na Mama yake anaishi Dar es Salaam kutokana na kutengana na Mumewe.
Mwendesha mashtaka wa Serikali Vincent Masalu aliiomba Mahakama kutoa adhabu Kali ili iwe fundisho kwasababu Mtuhumiwa amemuharibia Mtoto huyo maisha yake kisaikolojia lakini pia vitendo hivyo vimezidi kuongezeka Mkoani Iringa, Mahakama ilipompa nafasi ya kujitetea Mkoko hakuwa na chochote cha kuongea hivyo Mahakama ikamuhukumu kifungo cha miaka 30 jela.