Mwanaume mmoja huko Houston Texas ameshtakiwa kwa kujifanya afisa wa polisi ili aweze kuingia kinyemela kwenye Tamasha la Nne kumtazama Megan Thee Stallion akitumbuiza.
Trayvone Lil Darus Stevenson, 28, alikamatwa na kushtakiwa kwa kujifanya mtumishi wa umma siku ya Ijumaa baada ya kudaiwa kuvaa fulana ya “Polisi K-9” na kujitambulisha kama usalama kwenye hafla hiyo aliyetakiwa kufanya kazi kwenye tamasha hilo.
Mawakili walifichua kuwa Stevenson anafanya kazi kama kinyozi na hana sifa kama afisa yeyote, kama ilivyoripotiwa na ABC13.
“Megan Thee Stallion ni msanii mashuhuri anayejulikana haswa hapa Houston, lakini hii bado ni kesi ya uhalifu huwezi kwenda na kujifanya afisa ili kuingia katika eneo la tamasha,” mwendesha mashtaka Mathew Jackson aliambia chombo hicho.
Stevenson alishikiliwa katika Gereza huko Harris mwishoni mwa wiki, lakini jaji aliamuru kutolewa kwa dhamana ya $20,000. [mil 40]
Hana rekodi ya uhalifu ya hapo awali, na Stevenson aliachiliwa muda mfupi baada ya kusikilizwa.