Kiongozi mpya wa Hezbollah kutoka Lebanon, Naïm Qasim, ametoa hotuba yake ya kwanza siku ya Jumatano OKtoba 30, 2024, siku moja baada ya kuteuliwa kama mkuu wa kundi linalounga mkono Iran, zaidi ya mwezi mmoja baada ya kifo cha Hassan Nasrallah katika shambulio la Israel.
“Mpango wangu wa utekelezaji ni mwendelezo wa mpango kazi wa kiongozi wetu, Sayyed Hassan Nasrallah,” Naim Qasim amesema katika hotuba yake ya kwanza iliyorekodiwa kama kiongozi wa Hezbollah, akiahidi kuendeleza “mpango wa vita ambao alitayarisha na uongozi” wa kundi linaloungwa mkono na Iran.
Hayo yanajiri wakati jeshi la Israel limesema limewaua wapiganaji kadhaa wa kundi hilo, huku wanajeshi wake wakiendelea na uvamizi katika maeneo kadhaa ya Hezbollah kusini mwa Lebanon.
Wanajeshi wa Israel wamegundua shehena kubwa za silaha, kuharibu mahandaki, kuwaangamiza magaidi na kuharibu mitambo ya kurushia makombora ya Hezbollah iliyokuwa imefichwa katika maeneo ya umma na yaliyolenga kuzishambulia jamii za Waisraeli.