Mahakama ya uhalifu mjini Dakar siku ya Alhamisi imemhukumu kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, anayetuhumiwa kwa ubakaji, kifungo cha miaka miwili jela kwa “rushwa kwa vijana”, na uamuzi ambao unamzuia kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2024, wakati mvutano wa kisiasa ukiendelea kushuhudiwa nchini humo.
Sonko, 48, alishtakiwa kwa kumbaka mwanamke ambaye alifanya kazi katika saluni mwaka wa 2021 na kutoa vitisho vya kuuawa dhidi yake. Anakanusha kufanya makosa na anasusia kesi mahakamani.
Kesi hiyo imezua maandamano yenye ghasia, huku wafuasi wa Sonko wakipinga mashtaka dhidi yake kuwa yanachochewa kisiasa, jambo ambalo serikali na maafisa wa haki wanakanusha.
Kwa upande mwingine mahakama imemuondolea mashtaka ya ubakaji na vitisho vya kifo.
Hata hivyo imemhukumu mtuhumiwa mwenza wa Bw. Sonko, Bi. Ndèye Khady Ndiaye, mmiliki wa saluni ambapo Bw. Sonko alishtakiwa kwa kumdhulumu mfanyakazi mara kadhaa, kifungo cha miaka miwili gerezani.
“Jaji ataomba mamlaka kwa vyombo vya usalama kumpeleka jela,kwani macho yote yapo kwenye nyumba ya Ousmane Sonko anasema anaishi karibu na kizuizi cha nyumbani ambapo kuna ulinzi mkali karibu na nyumba yake. Hatua inayofuata ni kujaribu kumtoa nje ya nyumba yake na kumpeleka jela.”
Haijabainika mara moja jinsi hukumu hiyo ingeathiri ustahiki wake wa kupiga kura mwaka ujao. Kanuni za uchaguzi za Senegal zinazuia watu waliotiwa hatiani kwa kosa la jinai kuwania nyadhifa za kisiasa.
Kando, Sonko anakata rufaa dhidi ya kifungo cha miezi sita kilichosimamishwa jela kwa kashfa.
Athari za hukumu hiyo tofauti kwa nia yake ya urais haziko wazi