Aliyekuwa Kiongozi wa Wanamgambo katika taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ntabo Ntaberi amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo ubakaji wa watu wengi.
Mahakama ya kijeshi ilimkuta na hatia ya mauaji, ubakaji, utumwa wa kingono na kuwasajili watoto walio chini ya miaka 15 katika jeshi lake.
Uamuzi huo ulitolewa baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo iliochukua takriban miaka miwili ambapo waathiriwa 178 walitoa ushahidi wao.
Umoja wa Mataifa(UN) unasema kwamba umauzi huo umeonesha ‘uzoefu wa kutenda uhalifu bila kujali una kikomo chake’.
‘Uamuzi huo unawapatia matumaini waathiriwa wa mzozo huo wa DRC, mateso waliopitia yamesikilizwa na kutambuliwa’, amesema Leila Zerrougui, mkuu wa ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa uliopo nchini DR Congo.