Kipa wa Paris Saint-Germain Sergio Rico hatimaye ataondoka hospitalini Ijumaa hii baada ya ajali iliyomsababishia kupata majeraha mabaya kichwani na kulazwa katika hali ya kukosa fahamu, hospitali ya Virgen del Rocio huko Seville ilisema.
Tukio hilo lilitokea wakati Mhispania huyo alipogongwa na mkokoteni wa nyumbu na farasi alipokuwa akishiriki katika hija ya kila mwaka Kusini mwa Uhispania mnamo Mei 28. Rico alipelekwa hospitalini mara moja.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 alitoka katika hali ya kukosa fahamu mnamo Juni 19 na aliruhusiwa kutoka chumba cha wagonjwa mahututi mnamo Julai 5.
Rico alikuwa kwenye benchi la PSG katika sare ya 1-1 dhidi ya Strasbourg siku moja kabla ya ajali hiyo na alipewa ruhusa na klabu hiyo ya Ligue 1 kwa ajili ya kuhiji.
tazama pia….