Michezo

Kipigo cha Brighton 2-1 chaiweka Arsenal kwenye rekodi mbovu Ulaya

on

Club ya Arsenal licha ya kumfukuza kocha wake Unai Emery kwa timu yake kuwa na mfululizo wa matokeo yasiofaa, Arsenal bado haijakaa sawa na imeendelea kuutafuta ushindi kwa shida katika michezo yake mbalimbali.

Arsenal wakiwa nyumbani usiku wa December 5 2019 walikuwa wenyeji wa Brighton katika mchezo wao wa 15 wa EPL msimu huu, licha ya sapoti kubwa ya mashabiki Arsenal wamepoteza kwa kufungwa magoli 2-1.

Magoli ya Brighton yakifungwa na Adam Webster dakika ya 36 na Neal Maupay dakika ya 80, huku goli pekee la Arsenal likifungwa na Lacazette dakika ya 51 ya mchezo huo ambao uliifanya Arsenal ishuke hadi nafasi ya 10 katika EPL kwa kuwa na point 19 na Brighton wakipanda hadi nafasi ya 13 kwa kuwa na point 18.

Game hiyo inaiingiza Arsenal katika rekodi mbaya Ulaya kwakuwa ndio timu pekee katika timu zinazotoka Ligi 5 kubwa Ulaya msimu huu, kuruhusu kupigiwa mashuti mengi 52 (On Target) kuliko timu yoyote, hiyo imetokea baada ya Brighton kupiga mashuti 9 (On target).

 

Soma na hizi

Tupia Comments