Rais wa Kenya, William Ruto ameruhusu uagizaji wa nafaka zinazozalishwa maabara ili kukabiliana na njaa inayowakabili mamilioni ya raia wa Kenya kutokana na ukame mkubwa ambao umeshuhudiwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 40.
Kenya ilipiga marufuku matumizi ya mbegu kwa hofu ya kusababisha athari za kiafya kwa watumiaji. Rais Ruto ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa ameridhia matumizi ya mbegu hizo kwasababu Kenya inahitaji “mazao yanayoweza kukabiliana na ukame, wadudu na magonjwa”.
Kenya na Marekani ziliingia makubaliano mapya ya ushirikiano wa kukuza biashara ya kilimo mnamo mwezi Julai mwaka huu huku ikitarajiwa Marekani yenye wazalishaji wengi wa chakula kinachotumia mbegu zinazozalishwa maabara itakuwa mkombozi kwa Kenya katika kukabiliana na baa la njaa.