Mbunge wa Jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ameishauri Serikali kutoa nusu degree kwa Wanafunzi wanaoshindwa kumaliza elimu ya Chuo Kikuu kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukosa fedha kwa ajili ya kuendelea na masomo yao.
“Mimi Mtoto wangu anatakiwa kupata degree kwa miaka minne ameishia miaka miwili, nimekosa hela ameshindwa amerudi nyumbani huyu tunamwitaje?, kwanini asipewe nusu degree kwasababu anayeamua degree sio wewe ni Mwajiri, ukinipa nusu degree Tajiri ndio atatoa maamuzi”
Tazama zaidi