Michezo

Kishindo cha Samatta EPL

on

Wakati kukiwa na fikra na mawazo kwa baadhi ya wadau wa soka kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta kuwa wachezaji wenzake wa Aston Villa hawampi pasi mara kwa mara uwanjani.

Samatta leo akicheza EPL kwa mara ya kwanza na dakika zote 90 kutokana na kuaminiwa na kocha wake Dean Smith, leo amefunga goli lake la kwanza dakika ya 70 baada ya kuutumia vyema mpira wa Davis uliyozuiliwa na beki.

Goli hilo limefungwa Aston Villa ikipoteza 2-1 dhidi ya AFC Bournemuth katika uwanja wa Vitality, Samatta akiweka rekodi 2 mtanzania wa kwanza kufunga goli EPL, kaifanya Tanzania taifa la 117 kuwa na mchezaji EPL.

Soma na hizi

Tupia Comments