April 29 2016 Kesi ya Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare iliahirishwa.
Sababu zilizotajwa kuahirishwa kwa kesi hiyo ilikuwa ni jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu baada ya kukatwa kwa rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.
Kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa leo May 3 2016 Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ambapo Jalada la kesi hiyo lilitegemewa kurudi leo lakini halijarudi hivyo kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 18 2016 watuhumiwa wamerudishwa rumande.
Aidha watuhumiwa walitakiwa kufika mahakama Kuu kwa ajili ya kuendelea na rufani ambapo baada ya kufika Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kuanza kusikiliza rufani hiyo May 5 2016.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIIKOSA HII YA DALADALA KUSANZA KUPITISHA ABIRIA DARAJA LA KIGAMBONI? UNAWEZA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI