April 01 2016 aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanibic tawi la Tanzania, Shose Sinare walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kosa la utakatishaji fedha.
Kesi hiyo imeendelea leo April 27 2016 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Mahakama imefutilia mbali shitaka la utakatishaji fedha lililokuwa linawakabili washitakiwa wote hivyo washitakiwa wamebaki na mashitaka saba.
Upande wa Jamhuri umekata rufaa mahakama kuu na kusababisha maamuzi ya kupewa dhamana kuahirishwa mpaka April 29 2016 ambapo mahakama itatoa maamuzi kama watuhumiwa watapewa dhamana, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
ULIIKOSA YA KAMISHNA MKUU WA ZAMANI TRA NA WENZAKE WALIPOFIKISHWA MAHAKAMANI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE