AyoTV

VIDEO: “Kaseja ana nidhamu ya hali ya juu, nimempa mapumziko ya siku 4”

on

AyoTV ilitembelea mazoezi ya club ya KMC ya Kinondoni inayojiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Ruvu Shooting, mazoezi ya KMC yalifanyika katika uwanja wa Bora Kijitonyama na kukosekana kwa wachezaji Juma Kaseja na golikipa raia wa Burundi Jonathan Nahimana.

Baada ya kuulizwa kukosekana kwa wachezaji hao, kocha mkuu wa KMC Jackson Mayanja alieleza kuwa Nahimana ni majeruhi wakati Juma Kaseja ameamua kumpa mapumziko ya siku nne.

Mayanja ameeleza kuwa ameamua kufanya hivyo ili kumpa muda wa kupumzika Kaseja ambaye alikuwa na timu ya Taifa lakini aliporudi tu alionesha nidhamu ya hali ya juu akitokea Airport moja kwa moja alienda kambini kuungana na wenzake.

AUDIO: BREAKING: MASHABIKI WA YANGA WANAOKWENDA MWANZA WAMEPATA AJALI

Soma na hizi

Tupia Comments