AyoTV

VIDEO: ‘Tumeteseka kiasi cha kutosha, watu wanakufa’-Susan Kiwanga

on

Hii ni kutokea Bungeni Dodoma ambapo wabunge walikuwa wakichangia bajeti ya Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano ambapo Mbunge wa Mlimba Susan Kiwanga ambaye alilieleza bunge kuhusu changamoto zilizopo jimboni kwake ikiwemo ubovu wa barabara inayosababisha vifo kwa baadhi ya wananchi wake.

Susan amesema…>>>‘Jimbo la Mlimba wajawazito wanataka kujifungua moyo unaniuma mimi, moyo unalia machozi, wakinamama wajawazito wanakufa kwa kushindwa kufika hospitali kutokana na ubovu wa barabara

Mimi mwenyewe nikienda jimboni kuna wakati utanitafuta hunipati, hakuna mawasiliano ya simu, mjini mnajenga hadi flyover nyie nini? Kwanini wenzenu mmetusahau? Leo usafiri wa kule ni trekta. Jamani hivi bado tupo dunia ya leo?’ –Susan Kiwanga

Video yake yote nimekuwekea hapa chini tayari…

VIDEO: Anachokiona Hussein Bashe kuhusu ujenzi wa reli mpya

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments