Mwimbaji wa Nigeria Kizz Daniel alivyofuatwa hotelini kwake na kuchukuliwa na Polisi Dar es salaam leo baada ya kutotokea kutumbuiza kwenye show iliyokua imeandaliwa na Str8up vibes jana usiku Dar es salaam kitendo kilichosababisha uharibifu na hasara kubwa.
Sababu ambazo hazijathibitishwa ni kuwa Kizz alishindwa kutokea ukumbini na kutumbuiza kutokana na begi lake la nguo kucheleweshwa na ndege huku yeye mwenyewe akikataa kununuliwa nguo mpya Tanzania, Ayo TV inafuatilia zaidi tukio hili ili kukupa taarifa kamili baadaye