Michezo

Messi alipoulizwa kwanini kamtoa Ronaldo katika list ya wachezaji bora duniani

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi amezichukua tena headlines wakati wa mahojiano yake, Lionel Messi alifanyiwa mahojiano na Radio 94.7 na kuulizwa kuhusiana na soka lakini aliulizwa kuhusiana na kuondoka kwa Cristiano Ronaldo katika Ligi Kuu Hispania LaLiga anamkumbuka.

“Ndio namkumbuka Cristiano Ronaldo ingawa ilikuwa ngumu kumuangalia akishinda mataji, ameipa LaLiga Heshima”>>> Lionel Messi alipoulizwa kuhusiana na list yake anayoamini ndio wachezaji bora duniani kwa sasa Lionel Messi alijibu hivi.

Sitaki kumshahau mchezaji yoyote lakini nafikiri ni Neymar, Kyliane Mbappe, Eden Hazard, Luis Suarez na Sergio Aguero, Sijamtaja Cristiano Ronaldo kwa sababu namuweka katika Kundi moja na mimi”>>>Lionel Messi

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ndio wanaotajwa kuwa wachezaji bora sana hususani, rekodi yao ya kuitawala tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or kwa miaka 10 mfululizo, huku wakiwa wanapishana na kila mmoja akifanikiwa kushinda tuzo hiyo mara tano.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments