Mix

Rais Magufuli kawaapisha wateule wengine wawili leo July 27 2016

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Bw. Oliva Paul Joseph Mhaiki kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Aidha, Rais Magufuli amemuapisha Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).

Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Mwenyekiti na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu July 15 2016, viongozi hao wanakuwa wa kwanza kuongoza Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) tangu Tume hiyo ilipoundwa kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu Namba 25 ya mwaka 2015 ikiwa na majukumu ya kusimamia na kuratibu masuala yanayohusu utumishi wa walimu.

NI KWELI RAIS MAGUFULI ANAKATAA USHARI? MZEE MAKAMBA KAFUNGUKA HAPA, UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments