Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: BREAKING: Lowassa amfata Magufuli IKULU (+video)
Share
Notification Show More
Latest News
Picha:Kutoka kwenye shangwe za Simba DAY uwanja wa Mkapa Dar es Slaam
August 8, 2022
Kizz Daniel kutotokea kwenye show, Str8upvibes watoa tamko
August 8, 2022
Watalii zaidi ya 30 watembelea maporomoko ya Maji Hululu
August 8, 2022
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 8, 2022
August 8, 2022
International Marathon yaacha historia Zanzibar
August 7, 2022
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Breaking News > BREAKING: Lowassa amfata Magufuli IKULU (+video)
Breaking NewsTop Stories

BREAKING: Lowassa amfata Magufuli IKULU (+video)

January 9, 2018
Share
2 Min Read
SHARE

Leo January 9, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri na ametaja baadhi ya maeneo ambayo kazi kubwa imefanyika kuwa ni elimu bila malipo, ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji, ujenzi wa viwanda na ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa.

Namnukuu Lowassa >>>“Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo,”

“Moja na kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira na kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira,”- Lowassa

“Stiegler’s Gorge ni kujenga ajira na mengine ya aina hiyo, lazima kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba tunajenga ajira,  jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha elimu katika mambo yako unayofanya, kwa kweli nakushukuru  Rais, you made my day” – Lowassa.

Rais Magufuli amempongeza Edward Ngoyai Lowassa kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali na amesema Lowassa ni mmoja wa viongozi ambaye kwa wakati wake ametoa mchango wake katika nchi.

President Magufuli amesema kuwa Lowassa ni mwanasiasa mzuri kwani hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita ambao naye aligombea kiti cha Urais, hakuwahi kumtukana.

“Ameniomba mara nyingi nikutane nae na leo nimekutana nae, tumezungumza mambo mengi, kwa ujumla Lowassa ni mwanasiasa mzuri na tuendelee kuwaenzi wazee hawa ambao kwa nyakati fulani walifanya mambo mazuri, kama alivyosema tumefanya mambo mazuri mengi.”– President Magufuli

“Ametaja miradi mbalimbali tunayotekeleza, ametaja mradi wa Stiegler’s Gorge utakaogharimu zaidi ya Trilioni 7, juu ya maji ambayo kwa bahati nzuri yeye alikuwa Waziri wa Maji na anafahamu tumefikia wapi, amezungumza juu ya umeme tulivyosambaza katika vijiji, elimu bure, huduma za hospitali na mengine” -President Magufuli.

You Might Also Like

Kizz Daniel kutotokea kwenye show, Str8upvibes watoa tamko

International Marathon yaacha historia Zanzibar

Nane Nane Morogoro, Shaka apongeza jitihada za Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Mfahamu Panya Kennedy anayebeba Camera kama Binadamu ‘Anarekodi Matukio vitani’ (video+)

Video: Kinyozi ahukumiwa Jela miaka 30, kosa kumpa mimba Mwanafunzi

TAGGED: TZA HABARI
Millard Ayo January 9, 2018
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article The weekend akerwa na ubaguzi wa rangi uliofanywa kwa mtoto wa Kiafrika
Next Article JPM IKULU: “Lowassa hakuwahi kunitukana hata siku moja” (+video)
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Picha:Kutoka kwenye shangwe za Simba DAY uwanja wa Mkapa Dar es Slaam
Mix August 8, 2022
Kizz Daniel kutotokea kwenye show, Str8upvibes watoa tamko
Top Stories August 8, 2022
Watalii zaidi ya 30 watembelea maporomoko ya Maji Hululu
Mix August 8, 2022
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 8, 2022
Magazeti August 8, 2022

You Might also Like

Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 7, 2022

August 7, 2022
Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 6, 2022

August 6, 2022
Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 5, 2022

August 5, 2022
Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 4, 2022

August 4, 2022
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?