fB insta twitter

‘Anyang’anywa U-DC Sekunde ya mwisho Ikulu’

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya stori ni hii kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Anyang’anywa U-DC sekunde ya mwisho Ikulu’

Gazeti la hilo limeripoti kuwa aliyekuwa mteule wa ukuu wa wilaya, Emile Ntakamulenga alipata taarifa sekunde za mwisho kabla ya kula kiapo cha maadili cha kutumikia wadhifa wa mkuu wa wilaya ya Serengeti, kuwa uteuzi wake ulitangazwa kimakosa.

Gazeti hilo limesema kuwa baada ya kukabidhiwa nakala za viapo kila mmoja akiwemo Ntakamulenga, sekunde chache kabla ya kuapa na kusaini viapo hivyo, ndipo zilipokuja taarifa mbaya kwa mteule huyo .

Nipashe limeendelea kueleza kuwa wakati kukiwa na utulivu wa hali ya juu kwenye ukumbi huo , ndipo kamishna wa tume ya maadili ya utumishi wa umma, Jaji mstaafu Salome Kaganda, alipotangaza kwamba kuna marekebisho ya wateule ambayo yamefanyika.

Jaji Kaganda alisema katika uteuzi huo jina la Ntakamulenga liliingia kimakosa hivyo nafasi yake imechukuliwa na Nurdin Hassan Babu ambaye kwenye orodha iliyotolewa na Ikulu June 26  2016 hakuwepo.

Unaweza kuzipitia hapa chini habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya leo June 30 2016 

ULIKOSA UCHAMBUZI W

A MAGAZETI JUNE 30 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments