fB insta twitter

‘Muuaji msikitini Mwanza alivyowaponyoka polisi’

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya stori iliyoripotiwa ni hii kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Muuaji msikitini awaponyoka polisi’

Gazeti hilo limeripoti kuwa jeshi la polisi mkoani Mwanza limesema mtuhumiwa wa ujambazi waliyemkamata kwa matukio mbalimbali ya uhalifu yakiwamo ya uporaji maduka ya miamala ya kifedha na mauaji ya watu watatu msikitini, Hamis Juma, ametoroka chini ya ulinzi mkali wa polisi wakati akiwapeleka mlimani kuwaonyesha wahalifu wenzake.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Ahmed Msangi alisema juzi mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Nyegezi, alikuwa mikononi mwa polisi akiwapeleka walipojificha wenzake katika mlima Kiloleli Nyasaka kata ya Kirumba wilayani Ilemela.

Msangi alisema baada ya polisi na mtuhumiwa huyo wa ujambazi kufika eneo la tukio saa 8:00 usiku ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika mlima huo walianza kurusha risasi kwa askari ambao walitaharuki na kujibu mashambulizi huku wakimsahau mtuhumiwa aliyewapeleka ndipo alipopata mwanya wa kutoroka.

Aidha alisema katika mapigano hayo, polisi walikamata bunduki aina ya shortgun iliyokatwa mtutu na kitako na risasi moja kwenye chemba iliyotupwa na majambazi hao.

Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya July 05 2016

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA JULY 5 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments