Top Stories

“Tumeridhia vituo vihamishwe na kupelekwa katika majengo ya umma” Ramadhani Kailima

on

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeridhia kuhamishwa kwa vituo 46 vya kupigia Kura katika kata tatu za Jimbo la Kinondoni zitakazofanya Uchaguzi mdogo wa Ubunge,  February 17,2018.

Mkurugenzi wa Uchaguzi  wa Tume Ramadhani Kailima amesema kuwa uamuzi wa NEC kuridhia kuhamishwa kwa vituo hivyo, umetokana na makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa Msimamizi  wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni na Vyama vya siasa kuhusu kuhamishwa kwa vituo hivyo vilivyokuwa kwenye nyumba za ibada, zahanati na maeneo ya majengo ya watu binafsi.

“Tumejiridhisha kuwa baadhi ya vituo katika Kata ya  Kigogo vilikuwa katika nyumba za Ibada na vingine kuwa katika maeneo yenye ufinyu wa nafasi hivyo tumeridhia vituo hivyo vihamishwe na kupelekwa katika majengo ya umma,” -Kailima.

MAZISHI JUMATATU: BADO HAIJULIKANI NI DINI GANI ITAMZIKA MZEE KINGUNGE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

 

Soma na hizi

Tupia Comments