fB insta twitter

Habari kubwa magazetini leo, mojawapo ni hii ya ‘Msaidizi wa Kitwanga Matatani bungeni’

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini, Moja ya story kubwa June 04 2016 kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Msaidizi wa Kitwanga matatani bungeni‘.

Gazeti hilo limeripoti kuwa siku chache baada ya Rais John Magufuli  kutengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani , Charles Kitwanga kutokana na ulevi, Naibu waziri wa Wizara hiyo, Hamad Yussuf Masauni, ameshtakiwa kwa uongozi wa bunge akidaiwa kutoa majibu ya dharau bungeni.

Nipashe limesema kwamba jana June 03 2016 mbunge wa Nkasi ‘CCM’, Ally Keissy alisimama na kuomba mwongozo wa Spika akidai Mhandisi Masauni amekuwa akitoa majibu ya dharau kwa wabunge.

Gazeti hilo limemnukuu Keissy kuwa alidai Naibu Waziri huyo amekuwa akitoa majibu ya kejeli na kiburi na kwamba wabunge wengi hawaridhishwi na majibu yake .

katika majibu ya msingi ya swali langu, wamesema serikali itakarabati majengo ya Kabwe, lakini anasema baadaye (kwenye swali la nyongeza) mbunge akarabati majengo ya Kabwe , si dharau hii?-Ally Keissy

hayo majibu yanaridhisha? anajibu kwa jeuri na kiburi, kusema kweli wabunge haturidhishwi na majibu ya Naibu Waziri, sikubaliani na majibu ya aina hii’:-Ally Keissy

ULIKOSA HII YA WABUNGE WA CCM WAKIPINGA SHINIKIZO WAPINZANI KUTAKA KUMUONDOA NAIBU SPIKA DK TULIA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI  

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments