Mix

Wabunge wengine wanne wa CHADEMA hatihati kutimuliwa kuhudhuria vikao vya Bunge

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya story kubwa June 06 2016 kwenye gazeti la Raia Tanzania ni hii yenye kichwa cha habari ‘Wabunge wengine kutimuliwa’

Gazeti la Raia Tnzania limeripoti kuwa wabunge wanne wote kutoka CHADEMA wako hatihati ya kutimuliwa kuhudhuria vikao vya bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma kutokana na kukabiliwa na tuhuma mbalimbali za bunge, huku Mbunge wa Bunda mjini Esther Bulaya, akitarajiwa kuongezewa adhabu kubwa zaidi ya anayoitumikia kwa sasa.

Gazeti hilo limesema kuwa habari za kuaminika kutoka ndani ya kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge zimewatajwa wabunge hao wa CHADEMA kuwa ni Mbunge wa Simanjiro, James Millya, Mbunge wa Viti maalum, Suzan Lymo, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

Gazeti hlo limeripoti kuwa wabunge hao kwa pamoja kwa nyakati tofauti, wanadiwa kufanya makosa tofauti ya kikanuni katika mkutano wa bunge la bajeti linaloendelea Dododma, yakiwemo ya kuhamasisha vurugu ndani ya ukumbi wa bunge 

ULIKOSA DAKIKA 2 ZA WABUNGE WAKITOKA BUNGENI KUONYESHA KUTOKUWA NA KUTOKUWA NA IMANI NA NAIBU SPIKA TULIA ACKSON? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments