Duniani

Abiria kakosea mlango Ndege ikiwa angani, badala ya chooni akaenda kwenye mlango wa kutokea nje..

on

Ndege ya Shirika la KLM ilikuwa katikati ya safari kutoka Edinburgh kwenda Amsterdam, Uholanzi… ilibaki kidogo mambo yaharibike katikati ya safari.. abiria mmoja akakosea mlango, badala ya kufungua mlango wa kuingia chooni, yeye akaenda moja kwa moja kwenye mlango wa kutokea nje huku ndege ikiwa juu angani na safari inaendelea !!

Ingekuwa mlango huo ni mwepesi kuufungua kama mlango wa gari basi mambo yangekuwa tofauti, jamaa huyo James Gray, baada ya ndege kutua Uwanja wa Schiphol Airport alikamatwa na Askari na kuwekwa ndani kwa saa kadhaa alafu akaachiwa baada ya kupigwa faini ya Pound 440 ambazo ni kama Tshs. Milioni 1.4.

james-gray

Huyo ndio James Gray mwenyewe, na picha nyingine anaonekana alivyokamatwa na Polisi baada ya kutua uwanja wa Ndege.

Adhabu yake haijaishia hapo, jamaa kazuiwa pia kusafiri kwa Ndege za KLM kwa kipindi cha miaka mitano… Kwa vile yeye ni raia wa Scotland, ilibidi atumie usafiri wa Ndege nyingine kurudi kwao huku akijitetea kwamba yeye hata hakujua kwamba huo mlango ni wa kutokea nje.

Upande wa kushoto hapo ni mklango wa Choo ndani ya ndege, upande wa kulia ni mlango wa kutokea nje ya ndege.. hapo ndipo jamaa alipochanganyikiwa.

Upande wa kushoto hapo ni mlango wa Choo ndani ya ndege, upande wa kulia ni mlango wa kutokea nje ya ndege.. hapo ndipo jamaa alipochanganyikiwa.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments