Michezo

Klopp azidi kutamba EPL, tuzo za November na December kutawaliwa na Liverpool

on

Kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp amefanikiwa kutangazwa kuwa kocha bora wa mwezi December wa Ligi Kuu England kwa mara ya pili mfululizo, Klopp anashinda tuzo hiyo ikiwa ni mara ya pili mfululizo kushinda baada ya mwezi November kushinda pia.

Tuzo ya EPL ya mwezi kwa miezi miwili mfululizo imetawaliwa na Liverpool, mwezi November Klopp alishinda tuzo ya kocha bora wa mwezi EPL wakati mshambuliaji wake Sadio Mane akishinda mchezaji bora wa November, kwa December Klopp ameshinda tena tuzo hiyo na mchezaji bora kuibuka kwenye kikosi chake Alexander Arnold kuibuka mchezaji bora wa mwezi.

Kwa upande wa mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Son Heung-min ameshinda tuzo ya goli bora la mwezi December alilofunga dhidi ya Burnley, hii ni mara ya nne Klopp anashinda tuzo hiyo akiwa sawa na kocha wa Man City Pep Guardiola ambaye 2017/18 alishinda tuzo hizo mara nne ndani ya msimu mmoja kama ilivyo kwa Klopp msimu huu.

VIDEO: DIDA ALIACHWA SIMBA KISA KAOMBA MKATABA AKAUOSOME KABLA YA KUSAINI

Soma na hizi

Tupia Comments