Michezo

Klopp kajibu barua ya shabiki kinda wa Man United

on

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameandika barua ya kumjibu shabiki mtoto wa Man United Daragh mwenye umri wa miaka 10 ambaye aliandika na kueleza hisia zake kuhusiana na ubora wa Liverpool kwa sasa inayoonekana kushinda karibia kila mchezo.

Jurgen Klopp

Daragh ameandika barua hiyo na kumuomba Klopp kuwa haruhusu Liverpool ifungwe hata mchezo mmoja kwani wakiendelea kushinda kila mechi na wakashinda kwa mechi 9 mfululizo wataandika historia ya kipekee ambayo Daragh kama shabiki wa Man United itamuuzi sana.

Barua ya Daragh

Klopp alijibu barua hiyo na kumshukuru kijana Daragh kwa kutuma ujumbe huo lakini alieleza msimamo wake kuwa hilo haliwezi kutokea, yeye kuruhusu timu yake ipoteze.

Barua ya Klopp

VIDEO: MECKY AGOMA KUMTUPIA ZIGO LA LAWAMA TINOCO KIPIGO CHA 1-0 CHA SIMBA

Soma na hizi

Tupia Comments