Top Stories

Mtangazaji PJ aingia Jahazini kukamilisha Utatu mtukutu

on

Clouds Media Group imemteua Mtangazaji Paul James (PJ) kuungana na Gardner G Habash pamoja na George Bantu katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM baada ya kuwepo pengo la mtangazaji tokea Ephraim Kibonde afariki dunia March 7,2019.

Mtangazaji Paul James ambaye alikua kwenye kipindi cha Asubuhi  Power Break Fast sasa atatangaza rasmi kwenye kipindi hicho cha Jahazi ambacho hurushwa kila Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa kumi mpaka saa moja jioni. 

Kutokana na maamuzi hayo yaliyofanyika leo March 18,2018 baadhi ya wadau kwenye comments wameonekana kufurahishwa na PJ kuungana na kipindi cha Jahazi huku wengine wakisikitika kukiaga kipindi cha Power Break Fast.

Paul James (PJ) aliwahi kuwa kati ya watangazaji wa mwanzo kabisa kutangaza kipindi cha Jahazi, alikuwa yeye na Gadner pamoja na marehemu Kibonde, baadae PJ alihamia kipindi cha Power Breakfast.

VIDEO: ‘Siwezi kujichubua huo muda sina, Bongomovie wakongwe wanasumbua sana location’

Soma na hizi

Tupia Comments