Michezo

KMC yamuombea radhi Kabunda “Hakulenga kuidhihaki Yanga”

on

Club ya KMC imemuombea radhi mchezaji wake Hassan Kabunda kwa kitendo cha kushangilia na kinyago usoni baada ya kuifunga Yanga SC katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

KMC imeeleza Kabunda hakuwa na dhamira yoyote ya kuonesha vitendo vya ubaguzi wa rangi au dhihaka kwa Yanga kama baadhi ya watu walivyotafsiri.


Kama utakuwa unakumbuka vizuri kocha wa Yanga Luc Eymael alifutwa kazi baada ya kutuhuma za ubaguzi wa rangi na kuwaita Yanga nyani, sasa baadhi ya mashabiki wamekuwa wakitumia hiyo kama kejeli kwa Yanga kitu ambacho hakiruhusiwi michezoni.

Soma na hizi

Tupia Comments