Top Stories

Kampeni dhidi ya akina Baba wanaotegea malezi ya watoto yaanzishwa

on

Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, umekuja na kampeni ya wababa wa Kiswed na wababa wa Tanzania yenye lengo la kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na kuweka usawa katika malezi ya familia kati ya baba na mama.

Kampeni hiyo ambayo tayari imeshafanyika katika mikoa  mbalimbali ya Tanzania kwa sasa imefika katika Mkoa wa Tanga ambapo wananchi pamoja na viongozi wa dini wameipokea kwa mikono miwili .

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Katarina Rangnitt amesema kuwa wameamua kuanzisha kampeni hiyo ili kuweka usawa katika jamii ya Kitanzania kama ilivyo nchini Sweden  ili wazazi wote wawili washiriki katika malezi bora ya familia.

“Matokeo ya  tafiti yanaonyesha kwamba baba na mama wako sawa katika malezi ya familia  na Ninafikiri kwamba ili tujenge jamii nzuri na iliyo bora  zaidi ni lazima  ushirikiano uwepo  baina ya pande zote mbili kwani baba mzuri na mama mzuri ni yule ambaye anafuatilia maendeleo ya watoto.” -Katarina

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela amesema kuwa kampeni hiyo itasaidia kuwakumbusha watanzania wajibu wao wa kuwalea watoto kwa pamoja huku viongozi wa dini nao wakiunga mkono jambo hilo.

“Tunawajibu kujua watoto wanaendeleaje, je leo wamesoma siyo kusema mama anatosha na kwamba wamekula na wamelala.” -Shigela

Mambo 3 Kesi ya Rais Simba, Mashtaka yamebadilishwa, anatembea kwa kushikiliwa

Soma na hizi

Tupia Comments