Mix

Hizi picha ni za ajali ya daladala mbili iliyotokea leo Kinondoni Dar es Salaam

on

AW1A0145Ajali hii imetokea muda mfupi uliopita eneo la Kinondoni DAR, daladala mbili zimegongana eneo hilo katika Barabara ya Kawawa, katikati ya kituo cha Morocco Hotel na Kinondoni Mkwajuni.. zote mbili zilikuwa zimeongozana kutoka upande wa Kinondoni kuelekea Magomeni.

Askari wa Usalama Barabarani, Thomas L.M ambaye alikuwa eneo la tukio hilo amesema majeruhi wa ajali hiyo ni watu 18 ambao tayari wamefikishwa Hospitali kwa ajili ya matibabu na hakuna mtu aliyefariki.

Askari huyo pamoja na mashuhuda wamesema ajali hiyo imetokana na mwendo wa kasi uliosababisha daladala ya nyuma kuigonga nyingine iliyokuwa mbele yake.

AW1A0141

AW1A0145

AW1A0158

AW1A0159

AW1A0161

AW1A0162

AW1A0166

Hii ni gari ambayo imegongwa na daladala nyingine.

AW1A0172

AW1A0175

Gari za Breakdown zilifika kwa ajili ya kuondoa gari zilizopata ajali na kusababisha foleni kubwa eneo hilo.

AW1A0125

Mmoja wa majeruhi akiwa anapakiwa kwenye gari ya Kikosi cha Zimamoto.

Hapa utawasikia shuhuda wa ajali, dereva wa daladala iliyogongwa na Askari aliyekuwa eneo la tukio.

1. Shuhuda wa ajali hiyo, Mohammed Said.

2. Dereva wa daladala iliyogongwa.

3. Askari aliyekuwa eneo la tukio, Afande Thomas.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments