Siku chache zimepita toka lilipotokea tukio la kigaidi katika Chuo cha Garissa Kenya, kwenye tukio hilo wanafunzi 148 walifariki.. kingine kilichonifikia leo April 10 toka Kenya kinahusu uchunguzi uliofanyika kuonesha kwamba kuna dalili za uzembe ama matumizi mabaya ya madaraka wakati wa mikakati ya kupambana na wavamizi hao.
Taarifa za kwenye vyombo vya habari Kenya zinasema ndege ambayo ilitakiwa isafirishe maafisa wa Polisi kwenda kwenye Chuo hicho kwa ajili ya kupambana na wavamizi hao ilitumiwa kwa ajili ya safari binafsi ya familia moja ambapo kuna kiongozi mmoja anahusishwa kuruhusu ndege hiyo kufanya safari hiyo wakati ambao ilitakiwa kuwapeleka maafisa hao Garissa.
Rubani amesema ndege hiyo iliondoka katika uwanja wa ndege na kuwaacha makomandoo wa RECCE wakisubiri irudi kuwachukua na kuwapeleka Garissa kuwaokoa wanafunzi.
Nimekuwekea taarifa hiyo hapa iliyoripotiwa na kituo cha K24 bonyeza play kuisikiliza…
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook