Maajabu

Uliipata hii ya maajabu ya mbuzi huyu kutoka Kenya?

on

DSC00655
Mbuzi mmoja katika Kijiji cha Kakanjuni Kenya amezaa mbuzi mwenye vichwa viwili vilivyoungana huku akiwa na midomo miwili, tukio hili limewashangazawengi walioshuhudia huku wengine wakihisi kwamba mbuzi huyo ni mkosi.

Kahaso Ngumbao ambaye ndio anamfuga mbuzi huyo alitarajia mbuzi huyo angezaa mapacha kama kawaida yake lakini imekuwa tofauti, Wanakijiji walitaka kumuua kwa madai kuwa ni mkosi kutokana na mila za jamii hiyo.

Kwa sasa mwenye mbuzi huyo kuamua kumpeleka mbuzi wake Makao makuu ya Kilimo kwa ajili ya kumhifadhi wanakijiji wasimuue.

MbuziVichwaViwili

Nilikuwa natafuta njia ya kupatia msaada wa huyu mnyama maana hawezi na nikiachiwa mimi huenda nikashindwa saa nyingine.. nikiachia watoto hawawezi kumlea vile ambavyo labda ningekuwa mimi mwenywe” — Kahaso Ngumbao

Afisa wa Kilimo, Wanyama na Samaki aliahidi kuwa Serikali ya kaunti hiyo itatafuta mahali mbadala na kumhifadhi mbuzi huyo.

Sikiliza taarifa hiyo hapa iliyoripotiwa na kituo cha K24 kwa kubonyeza play…

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments