AyoTV

VIDEO: Waziri Kigwangalla kayajibu maswali haya bungeni..kelele zikasikika

on

Mei 4 2016 Bunge limeendelea Dodoma ikiwa ni mkutano wa tatu, kikao cha kumi na mbili ambapo katika kipindi cha maswali na majibu Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Hamisi Kigwangalla alikuwa akijibu maswali ya wabunge.

Baadhi ya maswali ni pamoja na Mbunge Mgeni Jadi Kadika viti maalum aliyeuliza..’Ugonjwa wa Myoma ni moja kati ya matatizo makubwa yanayoathiri akina mama kuzuia uzazi na kusababisha kansa ya kizazi pamoja na kupoteza maisha.

Katika moja ya swali la nyongeza aliloulizwa lilitoka kwa Mbunge wa Kaliua Magdalena Sekaya ambaye aliuliza..

Tunalotatizo kubwa sana la uzazi Tanzania, ndoa nyingi zinavunjika kwasababu wakinamama wanashindwa kupata mimba, Je, Naibu Waziri haoni kama ugonjwa wa Fibroid ni tatizo kubwa? ‘

Hapa Naibu Waziri Kigwangalla kayajibu maswali yote ambapo baadae baadhi ya Wabunge wakaanza kupiga kelele..

ULIZIKOSA HIZIDAKIKA 6 ZA MBUNGE KANGI LUGOLA KUHUSU WAKULIMA HEWA NA KAMPUNI ZA WAHINDI?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments