Top Stories

RAMSEY NOUAH: amkumbuka marehemu Kanumba, kutembelea kaburi lake kesho

on

Muigizaji maarufu wa Nollywood kutoka nchini Nigeria Ramsey Nouah ambaye kwa sasa yupo Tanzania amesema kuwa anamkumbuka msanii wa Bongo movie marehemu Steven Kanumba kwa sababu ndiye aliyejenga ushirikiano kati Nollywood na Bongo movie.

“Nimemkumbuka Kanumba ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kunileta Tanzania na kushirikiana naye kwenye filamu kadhaa, sitaweza kumsahau alikuwa ni mtu mzuri aliyependa udasisi na kujifunza,” – Ramsey

Ramsey amesema kesho Jumamosi ataenda kutembelea kaburi la Marehemu Kanumba na kuwaomba Watanzania waungane naye.

“Nawaomba Watanzania muungane nami katika kuweka maua na kuwasha mshuma kwenye kaburi la marehemu Kanumba,” – Ramsey

Ramsey na Kanumba waliigiza katika movie ya Devils Kingdom.

TAMKO LA BASATA KUHUSU KAULI YA JPM JUU YA VIDEO ZA BONGO, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments